NA MWAJUMA JUMA

WAPANGAJI wa makontena timu ya Bandari FC wanazidi kujiimarisha katika michuano ya Wara Ndondo cup baada ya juzi kushinda bao 1-0 dhidi ya Pablo Combine.

Mchezo huo ambao ni mwendelezo wa michuano hiyo ulichezwa uwanja wa Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Katika mchezo huo Bandari ambayo mechi iliyopita ilishinda kwa idadi kama hiyo dhidi ya Hawasemituu, hadi inakwenda mapumziko ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0.Bao hilo la pekee lilifanikiwa kuwekwa kimiyani na Khamis Bilali Denge dakika ya 25.