PARIS, UFARANSA

ALIYEKUWA kamishna wa Umoja wa Ulaya na kiongozi wa mazungumzo ya Uingereza kwenye mchakato wa Brexit, Michel Barnier, ametangaza kuwa anapanga kugombea urais nchini Ufaransa kupitia chama cha Republican katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Barnier alitangaza hayo kupitia televisheni ya TF1.Alisema kuna changamoto zinazowakabili katika nyakati muhimu, hivyo anatamani kuwa rais atakayeipatanisha Ufaransa.

Mwezi Januari Barnier aliteuliwa kuwa mshauri muhimu wa Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen.

Mwezi Desemba mwaka uliopita, alitangaza nia yake ya kurejea kwenye siasa za Ufaransa.Kabla ya kuhamia Brussels, Barnier alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa.