MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich imeibuka na ushindi wa mabao 12-0 dhidi ya Bremer SV katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Ujerumani.

Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Weserstadion, shujaa alikuwa kiungo Eric Maxim Choupo-Moting ambaye alitupia magoli manne (dk.ya 8,28,35 na 82).

Magoli mengine yalifunga na Jamal Musiala (dk.ya 16 na 48), Jan -Luca Warm aliyejifunga (dk.ya 27), Mali Tillman (dk.ya 47), Leroy Sane (dk.ya 65),Michael Cuisance (dk.ya 80), Bound Sarr (dk.ya 86) na Corentin Tolisso (dk.ya 88).

Katika mchezo huo, Bayern Munich walitawala katika kila idara ambapo kwa upande wa mashuti yaliyoelekea langoni walipiga 37 huku wapinzani wao wakipiga mashuti 7 na katika mashuti hayo 37, 21 yalilenga lango na wapinzani wao Bremer SV ni shuti moja lililenga lango.Umiliki wa mpira ilikuwa ni aslimia 68 kwa Bayern Munich na 32 kwa Bremer SV, pasi zilipigwa 612 upande wa Bayern Munich na 287 kwa Bremer SV.(Goal).