BRASILIA, BRAZIL

MAHAKAMA ya juu ya Brazil imeamuru rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro achunguzwe kwa madai ambayo hayajathibitishwa kwamba mfumo wa kupigia kura wa Brazil unagubikwa na udanganyifu.

Hukumu iliyotolewa na jaji Alexandre de Moraes ilitolewa baada ya Bolsonaro kuongeza ukosoaji wake kwa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya kielektroniki akisisitiza hakutofanyika uchaguzi mwaka ujao kama ilivyopangwa ikiwa hakutokuwa na  mageuzi.

Mfumo huo ulianzishwa mnamo 1996. Bolsonaro alisema uchunguzi dhidi yake uko nje ya mipaka ya katiba na ametishia kuchukua hatua nje ya katiba bila kufafanua.