MIAMI, Marekani
MCHEZAJI, Tom Brady amewashangaza wachezaji wenzake wa Soka la Mpira wa Amerika (NFL) kufuatia uamuzi wa kukubali kupunguzwa mshahara kwa asilimia 20.

Kama sehemu ya vita inavyoendelea dhidi ya ‘corona’ na athari zake kwenye mchezo huo, NFL imehimiza wachezaji kukubali sera mpya ambayo inapunguza kiwango cha mshahara kwa asilimia 20 kwa msimu wa 2021 na inasaidia kupunguza ‘presha’ kwenye ligi na wawekezaji.

Mpaka sasa tayari kuna kiwango fulani cha hasira katika ligi na timu zinawaomba wachezaji kufanya punguzo la mshahara kufuatia ‘corona’, lakini, hiyo ilidhihirika zaidi juzi ilipoibuka kuwa NFL ilikuwa imesaini makubaliano makubwa ya ‘televisheni’ ambayo yalikuwa yakiona thamani ya muwekezaji ikiongezeka kwa wastani asilimia 14.(AFP).