TOKYO, Japan
MIAMBA ya Brazil na Hispania zitakutana kwenye mchezo wa fainali ya soka ya wanaume ya Olimpiki baada ya miamba hiyo kuibuka na ushindi kwenye mechi za nusu fainali.

Brazil imefuzu hatua hiyo ya kucheza hatua ya fainali ya Olimpiki Tokyo 2020 baada ya kuifunga Mexico mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare 0-0 katika dakika 120.

Naye kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, Marco Asensio, alikwamisha mpira nyavuni kunako dakika za lala salama ya 115 na kuipa nafasi Hispania kufuzu hatua ya fainali.
Ni fainali ya kwanza kwa Hispania ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2000.
Mchezo huo utachezwa Agosti 7.(AFP).