LONDON, England
KLABU ya Bournemouth imekamilisha kusainiwa kwa beki wa kati wa zamani wa England, Gary Cahill kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Cahill (35), anajiunga na ‘Cherries’ kwa uhamisho wa bure baada ya kumaliza mkataba wake na Crystal Palace mwishoni mwa msimu uliopita.Anaweza kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na klabu hiyo nyumbani dhidi ya Blackpool kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza leo.

“Nimefanya uamuzi ambapo ninahisi hii ndio mahali pazuri zaidi kwangu kuwa katika hatua hii ya taaluma yangu”, alisema, Cahill.”Niliwasiliana na meneja (Scott Parker) mara kadhaa wakati wa msimu wa joto, kwa hivyo nilijua alitaka kunileta kwenye klabu na ninatarajia kuanza”.

“Nilitaka kitu cha kunipa changamoto na hii ni tofauti kabisa. Nadhani imekuwa kama miaka 17 tangu nilipocheza kwa mara ya mwisho daraja la kwanza kwa mkopo.
Cahill anakuwa mchezaji wa meneja wa Bournemouth, Parker, kusainiwa tangu kuteuliwa kwake mnamo Juni.

Kiungo, Emiliano Marcondes, kipa Orjan Nyland na mlinzi wa mkopo wa Leeds United, Leif Davis pia wamejiunga na ‘Cherries’.Cahill amecheza karibu mechi 400 kwenye Ligi Kuu England akiwa na Aston Villa, Bolton, Chelsea na Crystal Palace.(BBC Sports).