NA MADINA ISSA

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee CHADEMA, Hashim Juma Issa, bado Serikali ina wakati mzuri wa kuhakikisha tozo mbali mbali kwa wananchi zinakuwa za viwango vya chini, na badala yake watumie rasilimali mbali mbali ziliomo nchini ambazo zinaweza kusaidia ukuaji wa mapato ya Serikali.

Hayo aliyasema wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, huko Makao Makuu ya Chama hicho Kikwajuni Mjini Unguja.

Alisema Serikali bado ina nafasi ya kuitumia sekta ya kilimo kukuza uchumi wake kwani ina uwezo wa kuleta mabadiliko yatayosaidia kukuza pato la taifa.

“Lakini pia sekta ya ufugaji, Uvuvi wa bahari kuu, Madini Bandari zote hizi zinaweza kuzalisha pesa nyingi tu pindi serikali ikijipanga vyema katika kuzimarisha kisasa zaidi, kuliko kuangalia njia ya kuwaongezea kodi wananchi tu ambao kipato chao ni kidogo”alisema.