NA ZAINAB  ATUPAE

ZANZIBAR Milling Combine imeondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cossovo katika muendelezo wa mashindano ya elimu bila malipo ya vyuo vya Amali.

Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Amaan A majira ya saa 2:00 asubuhi.Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko hakuna iliofanikiwa kuzifumua vyavu za mwenzake.

Kurudi kumalizia kipindi cha pili timu hizo zilionekana kuingia na kasi kubwa,huku kila mmoja kufanya mabadiliko na kuingiza wa wachezaji kuwekwa sawa vikosi vyao.

Dakika ya 77 Juma Makame wa Zanzibar Milling Combine alifunga bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo huo.