KABUL, AFGHANISTAN

MKUU wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ameingilia tena masuala ya ndani ya Afghanistan sambamba na kufumbia jicho jinai zilizofanywa na Marekani na waitifaki wake wa Ulaya nchini Afghanistan.

Josep Borrell amedai kuwa kuna haja ya kurejeshwa usalama huko Afghanistan na kwamba jamii ya kimataifa inazitaka  pande zinazozozana nchini humo kuwawezesha raia wa kigeni na wa Waafghani kuondoka nchini humo kwa amani.

Mkuu wa Siasa za nje wa Umoja wa Ulaya ameongeza kuwa, Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi wanachama wa umoja huo wanafanya mkutano kwa njia ya intaneti kujadili hali ya mambo ya Afghanistan.

Bila ya kuashiria jinai za Marekani na waitifaki wake wa Ulaya huko Afghanistan sambamba na kuongezeka mashambulizi ya kundi la Taliban nchini humo, Borrel alitaka kusitishwa mara moja mashambulizi ya Taliban.

Zaidi ya nchi 60 duniani zimetoa taarifa ya pamoja na kueleza kuwa raia wa nchi za nje na Waafghani wanaotaka kuondoka nchini Afghanistan wanapasa kuruhusiwa kuondoka na viwanja vya ndege na vivuko vya mipakani vinapasa kufunguliwa na kubakia wazi.

Idadi kubwa ya wananchi wa Kabul walivamia uwanja wa ndege wa Kabul wakitaka kukimbia nchi baada ya kundi la Taliban kuidhibiti miji kadhaa ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu, Kabul.