LONDON, England
KIUNGO wa Liverpool, Fabinho, amesaini mkataba mpya utakaomuweka Anfield hadi mwaka 2026.

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, amecheza mechi 122 akiwa na wekundu hao alitumia muda mwengine kucheza kati kati ya safu ya ulinzi msimu uliopita kwa sababu ya matatizo ya kuumia kwa baadhi ya wachezaji.

Anamfuata beki mwenzake wa pembeni wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold, ambaye pia alisaini mkataba mpya wiki iliyopita.

“Ni kile nilichokitaka, kubakia katika klabu hii, kuichezea Liverpool, nina furaha”, alisema.
“Misimu hii mitatu iliyopita nimefurahia hapa. Nilijifunza mengi na meneja, na wafanyakazi wote, na wavulana pia.

“Tulifanikiwa vitu pamoja na kwangu mimi nadhani ni mahali pazuri pa kuwa, mahali pazuri pa kuendelea kukua, kuendelea kujifunza kutoka kwa wafanyakazi, kutoka wa wavulana.”(BBC Sports).