WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibar leo Jumapili, kama tunavyojua kuna safu maalumu ya mapishi, urembo na ile ya kinga au tiba ya kutumia mitishamba, mbogamboga na matunda.

Hivyo katika safu hii ya tiba asilia leo nimewatayarishia namna hiliki inavyofanya maajabu kwa baadhi ya matatizo mwilini kwa maana ya tiba.

Hili matra nyingi katika jamii zetu ni kiungo maalumu inayotiwa kwenye vyakula vingi ikiwemo mbagmboga, n ahata baadhi ya nyama kutegemea na mtu nini anataka kufanya.

Aidha hutumika sana kwnye vyakula vilivyo na mnasaba wa ungu iwe wa ngano wau wa aina nyengine yoyote.

Hiliki ni kiungo maarufu Sana nchini India, lakini hata katika nchi zetu kiungo hichi kimekuwa kikitumika kuongeza ladha katika vyakula na vinywaji mbali mbali pamoja na dawa kwa wagonjwa!

Aidha ina chanzo kizuri cha madini mwilini kama vile madini ya pottassiun, calicium,sulfur, iron pamoja na manganese.

Pia hiliki ina utajiri wa vitamins vingi sana ambavyo ni muhimu sana katika afya yetu ya mwili, vitamini inayo patikana katika hiliki ni kama vile vitamin A,B na C, Niacin, na Riboflavin.

ZIFUATAZO NI BAADHI YA FAIDA ZA HILIKI KIAFYA:-
Kuondoa harufu mbaya katika kinywa.

Hiliki ina viashiria ambayo vinaweza kuuwa vijidudu vinavyosababisha harufu mbaya katika kinywa.

Tafuna hiliki kila baada ya mlo ili kuacha kinywa chako kikiwa fresh na harufu nzuri.Sukutua kinywa chako kwa maji ya vuguvugu ya hiliki mara mbili kwa siku, ili kuondoa tatizo la harufu katika kinywa.

Hiliki Inaimarisha afya ya mfumo wa kusaga na kusharabu chakula na pia inachochea uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kuyeyusha vyakula vyenye mafuta mengi mwilini hii usaidia kupunguza gesi tumboni, kuondoa kiungulia na kutibu maumivu ya tumbo.Pendelea kutia hiliki katika vyakula au kunywa sana chai ya hiliki kuhimarisha usagaji wa chakula

Hiliki inasaidia kuleta hamu ya kula:-

Kutokana uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kunyeyusha vyakula vya mafuta na virutubisho vingine pamoja na kuondoa gas vitu ambavyo vinachangia kuondoa hamu ya kula
Tia unga wa hiliki katika supu au tafuta mbegu zake ili kurudisha hamu ya kula.

Hiliki inasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na kuzibua mirija ya hewa hivyo kuwapa unafuu wenye matatizo ya pumu, na matatizo mengine ya upumuaji.

Tumia hiliki kwa kutafuna kwa kiasi au kwa kunywa kusaidia matatizo ya pumu Kama vike kifua kubana na kukohoa.Hiliki inaondoa maumivu ya kichwa yanayotokana na tatizo la usagaji wa chakula.Kunywa kikombe kimoja cha chai ya hiriki kuondoa maumivu ya kichwa.