NA ZAINAB ATUPAE

FAINALI ya soka ya mashindano ya Chilo Shaban ndondo Cup inatarajiwa kupigwa leo huko uwanja wa skuli ya Uzini wilaya ya Kati Unguja.

Fainali hiyo itachezwa kati ya Mpapa na Bambi ya Kusini majira ya saa 10:00 jioni.Akizungumza na  gazeti hili mratibu wa mashindano hayo Mohamed Othman Mohamed,alisema zawadi mbali mbali zitaolewa kwa bingwa,makamu bingwa na mshindi wa tatu.

Alisema mbali na zawadi bingwa anatarajia kuondoka kwenda jijini Dodoma kufanya ziara  maalum.

Alisema ziara hiyo itaaandaliwa na mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo,hivyo aliwataka mashabiki kufika uwanjani kwa wingi siku ya fainali.

Alisema kabla ya fainali hiyo watafanya bonaza la michezo mbali mbali ikiwemo kufuta kamba,mbio za magunia na mpira wa miguu.