NA ABDI SULEIMAN

WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Lela Mohamed Mussa, amewataka akinamama ksiwani Pemba kuendelea kujiunga katika vikundi vya maoezi ili kuweza kuweka sawa miili yao, pamoja na kujiepusha na maradhi mbali mbali nyemelizi.

Alisema suala la ufanyaji wa mazoezi ni jambo la muhimu kwa watu wote, hivyo wanawake wanapaswa kujinga katika vikundi hivyo vya mazoezi, kwani ufanyaji wa mazoezi unamsaidia mwanamazoezi kuweka mwili wake sawa.

Waziri Lela aliyaeleza hayo katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya michezo kwa timu zilizomo ndani ya jimbo la Ole hivi karibuni.

Alisema kufanya mazoezi kunasaidia kujenga mwili imara na wenye nguvu, pamoja na kumuepusha mwanamichezo na maradhi nyemelezi.

“Mazoezi ni moja ya jambo muhimu, linamsaidia sana kuweka mwili sawa, ndioma akinamama huhimizwa sana kushiriki katika mazoezi kwa kusaidia kujengwa afya zao”alisema.

Aidha aliwasihi wanawake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mazoezi, kwani mazoezi yanaunda umoja, mshikamano na ufungu ndani yake.

Kwa upande wao akinamama waliokabidhiwa jezi za mazoezi walimshukuru waziri huyo, kwa kuwakumbuka wanawake katika suala zima la kufanya mazoezi.

Walisema kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakisahaulika katika suala la kupatiwa vifaa vya mazoezi, ikizingatiwa wanawake nao wanaumuhimu mkubwa katika hilo.