BARCELONA, Hispania
MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Ansu Fati amerejea mazoezini na kikosi cha kwanza cha klabu kufuatia kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na maumivu.Yoso huyo mwenye umri wa miaka 18 alikosa nusu ya pili ya msimu wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ baada ya kuumia goti la kushoto mwezi Novemba 2020.

Nyota huyo alipata jeraha wakati wa mechi ya ushindi wa magoli 5-2 wa Barcelona dhidi ya Real Betis huko Camp Nou, na baadaye akafanyiwa operesheni tatu.
Lakini, mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anakaribia kurudi uwanjani baada ya kupigwa picha tena kwenye uwanja wa mazoezi wa Barcelona wa Ciutat Esportiva Joan Gamper jana.

Ingawa hatopatikana kwenye mchezo wa ‘La Liga’ wiki hii dhidi ya Getafe, anaweza kuwa kwenye safari ya Barcelona kwenda Sevilla mwezi Septemba 11.

Mshambuliaji huyo alikua mfungaji mdogo zaidi katika historia ya Barca wakati alipofunga dhidi ya Osasuna mwezi Agosti 2019 akiwa na umri miaka 16 na siku 304.Fati aliongeza magoli mengine 12 katika mechi 42 kwenye mashindano yote ya ‘Blaugrana’, ambayo alijiunga akiwa na umri wa miaka 10.

Kijana huyo aliyezaliwa Guinea-Bissau amecheza mara nne kwenye timu ya Hispania, na alifunga bao lake la kwanza la kimataifa dhidi ya Ukraine mwezi Septemba 2020.(Goal).