ZASPOTI
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema, klabu hiyo imekuwa ikihitaji huduma ya mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane, lakini, hawajafikiria juu ya kumsajili, Lionel Messi.
Mabingwa hao wa England walikamilisha uhamisho wa kiungo mshambuliaji raia wa England na Aston Villa, Jack Grealish kwa dau la pauni milioni 100 huku wakihitaji pauni milioni 160 kukamilisha uhamisho wa Kane.

“Tunavutiwa naye, lakini, kama Spurs haiko tayari kuzungumza ni ngumu kumsajili”, alisema, Guardiola ambaye mpaka sasa amefanya usajili wa mchezaji mmoja tu.
“Ni mchezaji wa Tottenham, hivyo, tunahitaji waonyeshe ushirikiano kama itashindikana basi. Kama watakuwa wazi ManCity na klabu nyengine zinaweza kumsajili”.

Kane ambaye ni nahodha wa England, amefunga jumla ya magoli 221 akiwa na Tottenham ambapo ameshinda kiatu cha dhahabu mara tatu, karibuni alishinda msimu wa 2020/21.
Akizungumzia kuhusu kuondoka kwa Messi huko Barcelona, kocha huyo alisema, hakuamini wakati anapata taarifa hiyo.
“Kila mmoja ilikuwa ni taarifa ya kushangaza, hata mimi niliduwazwa”, alisema.(Goal).