MUNICH, Ujerumani

ERLING HAALAND anasisitiza anajivunia kuichezea Borussia Dortmund, wakati Chelsea inakaribia mpango wao wa kumsajili Romelu Lukaku.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway alikuwa chagu la kwanza la Chelsea msimu huu wa joto, lakini Dortmund imekuwa ikisisitiza wakati wote wa kiangazi kwamba mshambuliaji huyo angebaki nao angalau msimu mwingine.

Chelsea pia walivunjika moyo kwani  makubaliano ya Haaland yalitarajiwa kugharimu zaidi ya pauni milioni 150.

Badala yake, mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa wamemgeukia Lukaku na sasa wako mbioni kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 97.5 kwa mshambuliaji wao wa zamani.

Wakati huo huo, Haaland, hakutoa dalili yoyote kwamba anataka kuondoka Dortmund na mchezaji huyo 21, alionyesha mapenzi yake kwa klabu baada ya ushindi wao wa 3-0 dhidi ya SV Wehen Wiesbaden katika raundi ya kwanza ya DFB Pokal.

Mkuu wa mpira wa miguu wa kikosi cha kwanza cha Dortmund, Sebastian Kehl, pia alisisitiza msimamo wa klabu kwamba Haaland hauzwi msimu huu wa joto.