NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya soka ya Ikulu FC imeaga mashindano ya Yamle Yamle licha ya kushinda mchezo wake uliochezwa juzi.

Ikulu ilishuka katika dimba la Amaan nje kucheza na Urafiki FC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kukamilisha ratiba kwa kundi L, ambalo limetoa timu mbili zilizotinga hatua ya 32 bora.

Timu ambazo zimetinga hatua hiyo kutoka kundi hilo ni Bridge Star na Nyumba mbili ambazo zilikutana katika uwanja wa Magirisi na kutoka sare ya kutofungana.