YERUSALEMU, ISRAEL

MAHAKAMA ya juu ya Israel imeahirisha uamuzi kuhusu kesi ya rufaa ya familia nne za Kipalestina zinazokabiliwa na kitisho cha kutimuliwa na Mayahudi kutoka kitongoji cha Sheikh Jarrah huko Jerusalem Mashariki.

Wapalestina hao walisema walipewa fursa ya kubaki katika maeneo yao kama wapangaji wanaolindwa ambao watatambua umiliki wa Israel wa makaazi hayo na kulipa kodi ya mwaka, lakini wakakataa.

Kusikilizwa kwa kesi hiyo ni sehemu ya vita vya kisheria vya miaka minne na mashirika ya kiyahudi yanayojaribu kukomboa mali zilizokuwa zikimilikiwa na wayahudi huko Jerusalem Mashariki kabla kuundwa kwa taifa la Israel mnamo 1948.

Wapalestina hao wanasema Jordan iliwapa makaazi eneo hilo baada ya kutimuliwa kutoka miji yao katika maeneo yaliyokuja kuwa sehemu ya Israel na nyaraka mpya kutoka Jordan ziliwasaidia katika kesi yao.