PYINMANA, MYANMAR

JESHI la Myanmar limetangaza kuundwa kwa serikali ya mpito, huku mkuu wa jeshi, Jenerali Mwandamizi Min Aung Hlaing, akichukua wadhifa wa waziri mkuu.

Taasisi ya juu zaidi ya kufanya uamuzi ya jeshi hilo ambayo ni Baraza la Utawala la Taifa, ilitangaza kuundwa kwa serikali hiyo kwenye runinga ya serikali.

Baraza hilo lilieleza kwamba serikali ya mpito iliundwa ili kutekeleza shughuli zake haraka zaidi na kwa njia fanisi.

Lakini wafuatiliaji wa mambo wanasema dhamira ya hatua hiyo ni kuwapa viongozi wa mapinduzi mamlaka na kuhalalisha utawala wa kijeshi.