NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya soka ya JKU Academy imefanikiwa kuwa bingwa wa mashindano ya Vumbua Vipaji Cup baada ya kuichapa KVZ Academy mabao 5- 4 ya penalti.

Fainali hiyo iliotimua vumbi uwanja wa Mao Zedong B majira ya saa 10:00 jioni ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid.

Dakika 90 za mchezo huo zinamalizika hakuna timu iliofanikiwa kuzifumua vyavu za mwenzake na kulazimika kupigwa mikwaju ya penalti kupatikana bingwa wa mashindano hayo na kukabidhiwa zawadi.

Katika penalti hizo JKU iliondoka na penalti 5, huku KVZ iliondoka na penalti 4 na kukosa moja.

Kwamatokeo hayo bingwa JKU aliondoka na kombe na medali, huku KVZ makamu bingwa alipata medali na mchezaji bora alipata zawadi ya jezi ya mpira.