NA HAFSA GOLO
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Sera ,Utratibu na Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid Salum Mohamed, amesema Kamati za Kudumu za Baraza la Wakilishi, kuhakikisha zinasaidia kuongeza ufanisi ndani ya chombo hicho, na kuleta mageuzi ya maendeleo majimboni pamoja na kutimiza malengo ya serikali.
Waziri huyo akizungumza na Zanzibar Leo, baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Kudumu ya Viongozi Wakuu ya Baraza la Wawakilishi ofisini kwake Vuga mjini Unguja.
Alisema utendaji kazi mzuri wenye kufatilia kwa karibu utatuzi wa changamoto za wananchi kuchapakazi kwa bidii, ubunifu na utekelezaji mzuri wa majukumu ya kazi kwa utasaidia kuimarisha ndoto walizoziweka katika majimbo yao.
“Lazima viongozi na watendaji tuchape kazi kwa bidii huku tukibuni mbinu sahihi za uimarishaji wa maendeleo katika maeneo yetu ya kazi, hivyo tutaweza kutimiza mipango tuliojiwekea katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii”,alisema.