LONDON, England
MSHAMBULIAJI, Harry Kane, amethibitisha ataendelea kusalia katika klabu ya Tottenham msimu huu wa joto baada ya mchakato wa kuhamia Manchester City kushindikana.

Kane amebakisha mkataba wa miaka mitatu Spurs na alicheza akitokea benchi katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Wolves katika mechi yake ya kwanza tangu kurudi kutoka maandalizi ya msimu.

Mshambuliaji huyo amedhibitisha katika mtandao wake wa twitter kwamba atasalia katika msimu huu wa joto:

“Nilishangazwa kuona mapokezi kutoka kwa mashabiki wa Spurs na kusoma ujumbe mbalimbali wa kuniunga mkono katika wiki chache zilizopita.
“Nitabakia Tottenham msimu huu wa joto na nitazingatia kwa 100% kusaidia timu kupata mafanikio”(BBC Sports).