ZASPOTI
MASHABIKI wa muziki na watu wengine wengi duniani wanamtambua kwa jina R. Kelly, lakini jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, ambaye siku yake ya kwanza kuja duniani ilikuwa Januari 8 ya mwaka 1967 huko katika mji wa Illinois katika jimbo la Chicago nchini Marekani.
Kelly ni binaadam aliyejaliwa kuwa na vipaji vingi kwenye tasnia ya muziki, kwani ni bingwa wa kuandaa muziki kwa maana ya producer vile vile ni mwandishi mzuri wa mashairi.
Gwiji huyo pia ni miongoni mwa wataalamu mahiri wa kuimba aliyejaaliwa kuwa sauti nzuri akimudu sana miondoko ya R&B, nje ya muziki R. Kelly pia ni mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu ambapo aliwahi kuichezea timu ya Native of Chicago.
Alianza kujihusisha na shughuli za muziki mnamo miaka ya 1980 na mnamo mwaka 1992 alijiunga na kundi la muziki na miondoko ya R&B la Public Announcement, ambalo lilianzishwa mwaka 1991 hapo hapo Chacogo, Illinois.
Mbali ya R. Kelly kundi hilo lilikuwa na wanamuziki wengine wakiwemo Andre Boykins, Earl Robinson, Ricky Webster, Big Mel, Euclid Gray ambapo walitengeneza kundi lenye nguvu na lililojipatia sifa kwenye muziki nchini Marekani.
Kundi la Public Announcement, lilifanikiwa kutoa baadhi ya vibao vikali vilivyojipatia sifa kama vile “She’s got that vibe, Honey Love, Slow dance (Hey mr DJ), Dedicated, Body Bumpin (Ippie Yi-Yo) na Mamacita.
Baada ya kufanya hayo yote mnamo mwaka 1992, R. Kelly alitoa albumu yake ya kwanza akiwa kama Solo YA 12 PLAY, ambayo ilikuwa na nyimbo kali 12, Your Body’s Callin’ na Bump n’ Grind.
Nyengine ni Homie Lover Friend, It Seems Like You’re Ready na Freak Dat Body, I Like the Crotch On You, Summer Bunnies, For You, Back to the Hood of Things, Sadie, Sex Me Pt 1 & 2 na 12 Play. R.Kelly ndiye msanii wa pekee wa muziki nchini Marekani ambaye alisajiliwa kucheza mpira wa kikapu wa kulipwa mnamo mwaka 1997.
Mwanamuziki huyo pia alishirikiana kwa karibu kumuandikia nyimbo pia kuproduce nyimbo za wasanii wengi wakiwemo msanii Aaliyah Dana Haughton alimaarufu Aaliyah mwaka 1994 katika album yake ya Age Ain’t Nothing but a Number.
Mnamo mwaka 1996 alifanikiwa kushiriki katika tuzo za grammy kwa kuwandikia nguli ya pop duniani marehemu Michael Jackson wimbo wa “You are not alone” huku mwaka 2002 na 2004 R. Kelly alifanikiwa kutoa album yake aliyoifanya na Jay-Z na kuweza kutajwa kama mkali wa voco na wasanii kama Nas, Sean Combs, pamoja na mkali The Notorious B.I.G.
Lakini mnamo mwaka 2002 iliweza kumtokea habari mbaya ya kupata kesi ya kuwafanyia vitendo vibaya vya kingono mabinti wadogo 21, kesi inayomuumiza kichwa hadi hivi leo.
Mbali na hilo Recording Industry Association of America (RIAA) liliweza kumtaja R. Kelly kuwa ndio msanii aliyefanikiwa kuuza muziki wake nchini Marekani na duniani kote kwa kuuza zaidi ya kopi milioni 40 za album yake.
Mnamo mwaka 2011 R Kelly alitajwa kuwa ni miongoni mwa wasanii waliofanikiwa zaidi katika sanaa katika miondoko ya R&B kwa zaidi ya miaka 25.
Alitoa album 12 akiwa mwenyewe na kufanikiwa kuuza zaidi ya kopi milioni 75 katika kila wimbo duniani kote na kumfanya yeye kuwa ndio msanii wa R&B aliyefanikiwa zaidi kati ya miaka ya 1990.
Mwanamuziki huyo alifanikiwa kuingia katika orodha ya List of best-selling music artists na kufanikiwa kupewa jina la utani la King of R&B yaani Mfalme wa R&B duniani na mfalme wa Pop-Soul na kufanikiwa kuingia katika orodha ya wasanii wa Billboard katika miondoko ya R&B waliofanikiwa zaidi kwa zaidi ya miaka 25. na kuingia katika historia ya wasanii wa R&B waliofanikiwa.
Mbali na mafanikio hayo R. Kelly anamiliki baadhi ya tuzo zikiwemo Guinness World Records, Grammy Award, BET, Soul Train, Billboard, NAACP na The American Music Awards (AMAs).
Kuhusu familia R. Kelly ana familia na ana watoto watatu, mke wake Andrea Danyell Kelly ambaye alikuwa dansa alimuoa mwaka 1996 na mnamo mwaka 2006 waliachana.
Historia ya R. Kelly hainogi kuielezea pasi ya kuingiza kashafa kadhaa za ngono zinazomkabili kwani mnamo Februari 3 ya mwaka 2002 ilizuka habari mbaya ya kurubuni kingono mabinti waliochini ya miaka 18.
Video za kashfa hiyo zilisambaa bila kujua chanzo cha kusambaza habari hizo ni nani na zilianza kuonekana katika kituo cha Chicago Sun-Times, ambazo zilitoka siku tano baadaye yaani tarehe 8 mwezi huo Februari ya mwaka 2002.
Taarifa hizo zilimuumiza sana R. Kelly kwani alitakiwa kwenda kupafomu katika mashindano ya wazi ya Olimpic ambayo yalifanyika hapo nchini Marekani.
Katika moja ya mahojiano aliyoyafanya na kituo cha WMAQ-TV na MTV News, R. Kelly alisema,” Sio yeye aliyeonekana kwenye video zile” ingawa baadaye mwezi wa sita (June) alikuja kushitakiwa kutokana na kosa hilo.
Katika video hizo ingawa R Kelly alikataa lakini ziliwaonyesha mabinti hao wakifanyiwa vitendo hivyo katika nyumba ya R Kelly. Kelly alikamatwa Januari 2003 kwa mashtaka hayo. Mnamo Machi 2004, mashtaka haya yalipunguzwa.
Baada ya ucheleweshaji wa kusikilizwa kesi hiyo Oktoba 27 mwaka 2006, kata ya Cook, Illinois mahakama kabla ya kesi kusogezwa na kuwa tarehe kesi halisi itakuwa Februari 7, 2007.
Siku ya shauri hilo lilisikilizwa na mwanasheria wa Kelly ambaye aliiambia mahakamani kuwa mteja wake hakuhudhuria kwa sababu alifanyiwa upasuaji. Alitangaza pia kwamba Kelly akiwa katika hali nzuri na alitarajiwa kutolewa kutoka hospitali baadaye siku hiyo.
Mwanasheria wa Kelly alisema kwamba Kelly (ambaye hakuwa na hatia) angehudhuria tarehe ya pili ya tarehe 21 Februari 2007. Ilikuwa imetangazwa hapo awali na mahakama kuwa videotape ambayo inadaiwa ilionyesha Kelly kufanya vitendo vya ngono na mwanamke mdogo angeonyeshwa hadharani kama ushahidi katika kesi hiyo.
Hata hivyo, kesi hiyo ilikuwa imechelewa kutokana na migogoro juu ya wakati mkanda ulifanywa na kutoa muda wa matibabu kwa muhusika.
Baada ya kuanguka na kusababisha mifupa kuvunjika. Baadaye kesi iliwekwa tarehe ya Septemba 17 ilichukua muda wa miezi sita. Kesi ilianza rasmi Mei 20 na taarifa za ufunguzi kutoka kwa mashtaka na ulinzi.
Baada ya wiki mbili, kesi ya upande wa mashitaka imefungwa mnamo Juni 3 wakati wa ushahidi amefungwa mnamo tarehe 9 Juni. Baada ya siku ya maamuzi, Juni 13, jaji katika mahakama ya Chicago liligundua Kelly hakuwa na hatia ya makosa yote 14.