NA JOSEPH NGILISHO, ARUSHA
KESI ya Mgogoro wa Ardhi baina ya Kanisa la Christ Synagogue Ministries, lililopo Sakina jijini Arusha na wasimamizi wa mirathi Bernadette Changuru na Samweli Changuru inatarajia kuanza kusikilizwa Disemba 6, mwaka huu.
Shauri hilo, namba 57/2021 linasikikizwa na Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Arusha, Mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Gladness Kagaluki, ambapo mwishoni mwa wiki lilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa terehe ya kusikilizwa
Wakili wa upande wa mashtaka, Ismael Shallua alieleza mahakama hiyo kwamba shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa ,hata hivyo upande wa wajibu maombi ukiwakilishwa na Wakili Gwakisa Sambo walidai wapo tayari Kwa hatua za usikilizwaji .
“Mheshimiwa mwenyekiti shauri hili limekuja Kwa ajili ya kutajwa tulikuwa tunaomba muda mwingine Kwa ajili ya kusikilizwa”alisema Wakili Shallua.