MUNICH, Ujerumani
KIUNGO, Joshua Kimmich, ameongeza kandarasi yake na Bayern Munich hadi 2025, kulingana na tovuti rasmi ya klabu.Akiwa na uwezo wa kucheza kwenye safu ya kiungo au beki wa pembeni, Kimmich alijiunga kutoka RB Leipzig mwaka 2015 na amefanikiwa kushinda mataji 17 na Bayern ambayo inatafuta taji la 10 mfululizo la Bundesliga msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alisema, sababu muhimu zaidi ya kuongezwa kwa mkataba wake ni kufuata mapenzi yake kwa furaha kila siku huko Bayern.

“Juu ya hayo, familia yangu inahisi iko nyumbani hapa. Munich imekuwa nyumba ya pili”.
Ana taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, alishinda mwaka 2020 na mataji sita ya ‘Bundesliga’ mfululizo kutoka 2016 hadi 2021 na Bayern Munich.Kimmich amefungaa magoli 30 na usaidizi 73 katika michezo 264 ya Bayern Munich hadi sasa.Kiungo huyo wa ulinzi ana michezo 59 kwenye timu ya taifa ya Ujerumani, akizalisha magoli matatu. (AFP).