TOKYO, Japan

MWANARIADHA Eliud Kipchoge amesema ametimizi ndoto yake baada ya Mkenya huyo kuwa mwanariadha wa kwanza tangu 1980 kuhifadhi taji la mbio za Olimpiki Tokyo 2020.

Kipchoge, ni mtu wa tatu kushinda mbio za masafa marefu katika michezo ya Olimpiki na kukamilisha mbio hizo katika muda wa saa 2:38.

Mwanaridha huyo mwenye umri wa miaka 36 anayetambuliwa kama mkimbiaji bora zaidi, alivuka mstari dakika moja na sekunde 20 mbele ya Abdi Nageeye wa Uholanzi.

Katika mbio za kuwania taji la shaba mwanariadha wa Ubelgiji Bashir Abdi alimpiku Mkenya Lawrence Cherono.

“Nafikiria nimetimiza ndoto yangu kwa kushinda mbio za marathon kwa mara ya pili . Natumai sasa kusaidia kuhamasisha kizazi kijacho, ” Kipchoge alisema.

“Nina furaha kutetea taji langu na kuonyesha kizazi kijacho, ikiwa utaheshimu mchezo huo na kuwa na nidhamu unaweza kutimiza ndoto zako.”

Eliud Kipchoge alikua mwanariadha wa kwanza kukimbia mbio hizi kwa chini ya masaa mawili mnamo Oktoba 2019, ingawa wakati huo haikutambuliwa kama rekodi rasmi ya marathon duniani.

Hii ni medali ya nne ya Olimpiki kwa Kipchoge,ambaye alipata umaarufu wa kukimbia mbio hizo kwa muda bora zaidi wa chini ya masaa mawili mwaka 2019.

Kipchoge alishindwa katika mbio hizo mara ya kwanza ndani ya miaka saba huko London mwezi Oktoba, lakini alichukua alishinda tena mjini Sapporo, Japan, kabla ya kuingia kuonesha umahiri wake katika mbio hizo baada ya kukimbia kilomita 30.

Mkenya huyo  ambaye rekodi yake ya marathoni ni 2:01:39 alikimbia huko Berlin mnamo 2018 – alishinda shaba ya mita 5,000 mwaka 2004 na fedha mnamo 2008, kabla ya kushinda dhahabu yake ya kwanza ya Olimpiki huko Rio miaka mitano iliyopita.

Siku ya Ijumaa, Peres Jepchirchir wa Kenya alishinda mbio za marathon upande wa wanawake.