NA JOSEPH DIAVID
KOCHA wa timu ya Simba queens Hababuu Ali amewaomba watanzania kuwaunga mkono, ili iwakilishe vyema nchi kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya soka kwa wanawake ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Akizngumza kwenye kipindi cha michezo cha televisheni ya TBC1, alisema wanahitaji dua nyingi za watanzania, ili waweke historia kuwa timu ya kwanza kunyakua ubingwa wa michuano hiyo ambayo inafanika kwa mara ya kwanza.
Mashindano hayo yataanza kutimua vumbi kati ya Agosti 28 hadi Septemba 9 huko Nairobi Kenya yakizijumlisha timu nane ambazo ni mabingwa wa soka kwa ligi ya wanawake ndani ya nchi zao.
Simba queens imepangwa kwenye kundi A ikiwa pamoja na timu za PVP Fc (Burundi), Lady Doves WFC (Uganda) na FAD (Djibouti)
Mshindi wa jumla wa michuano hiyo atakwenda nchini Misri kushiriki ligi ya mabingwa Afrika kwa soka la wanawake akichuana na mabingwa wengine kutoka kanda tofauti.