LONDON, England
MANCHESTER City wataweka sanamu ya David Silva na Vincent Kompany nje ya uwanja wa Etihad kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Arsenal mwishoni mwa wiki.
ManCity iliagiza sanamu hizo kwa wawili hao ambao wanaonekana kama wachezaji wawili wakubwa katika historia ya klabu na baadaye itaongeza moja ya mshambuliaji wao wa zamani, Sergio Aguero.

Kompany alitumia miaka 11 kwenye klabu hiyo wakati Silva alikuwa Etihad kwa muongo mmoja na alisaidia kuibadilisha City kuwa moja ya timu bora nchini England.

Sanamu hizo zilizoundwa na msanii wa Uingereza aliyeshinda tuzo, Andy Scott, kazi zilizomalizika zitabakia kuwa siri hadi hapo zitakapowekwa wazi kwa umma wiki hii.
Scott alikutana na Kompany na Silva kwa sababu ya janga la ‘corona’ na kuwafanya kwenye studio yake huko Philadelphia.

Mwenyekiti, Khaldoon Al Mubarak alitangaza uamuzi wa kuwaheshimu wachezaji hao watatu mwaka 2019 kufuatia kuondoka kwa Kompany kwenda kuinoa Anderlecht.
“Bado ni ngumu kufahamu. Ninarudi mwanzo kabisa wakati nilisaini ManCity na hatukuzungumza juu ya sanamu wakati huo”, alisema, Kompany.

“Kuanzia siku ya kwanza ilikuwa kazi ngumu na kukaa imara kiakili na kimwili kushindana tu. Mwishoni mwa wakati wangu huko ManCity, unapewa heshima na kitu ambacho haukutarajia kabisa wakati wowote.”Baadaye, unatambua umekuwa sehemu ya kikundi maalum cha wachezaji kwa historia ya klabu na kuanza kwa kitu, lakini, ni ngumu kuelewa”.(AFP).