NA LAYLAT KHALFAN

MKUU wa Wilaya Magharibi A, Suzan Peter Kunambi, amewasisitiza wana vikundi vya mazoezi, kuwa wabunifu wa miradi ndani ya vikundi vyao.

Kunambi aliyaeleza hayo wakati akizindua kalenda ya klabu za mazoezi zoni C.Alisema kwa sasa vikundi vingi vya mazoezi vinakufa kutokana na kukosa ubunifu wa kuendeleza vikundi hivyo.

Aidha Kunambi aliwataka wanamichezo hususan zoni C kuendeleza umoja huo kwa maslahi ya afya zao na taifa kwa ujumla.

Aidha, uzinduzi huo ulioambatana na mbio kuanzia Bububu gengeni hadi katika viwanja vya Beit ras.Pia wanavikundi hao walifanya usafi wa mazingira na  kuchangia damu.

Naye Katibu Mtendaji wa Chama cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA), Khamis Akhui Khamis, aliwataka wanavikundi hao kujiunga na ZABESA, ili kuwa wanachama hai ndani ya umoja huo kwa lengo la kuimarisha na kuunganisha klabu za mazoezi.