BEIRUT, LEBANON

SERIKALI ya Lebanon imekubali kulipa maelfu ya familia masikini msaada wa pesa taslimu kwa dola za Kimarekani kutoka kwa mkopo wa Benki ya Dunia wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mzozo wa kiuchumi.

Uamuzi huo unatokea wakati Lebanon ikitarajiwa kuondoa kabisa ruzuku ya mafuta mwishoni mwa mwezi ujao hatua ambayo inatarajiwa kusababisha ongezeko la bei ya bidhaa muhimu nchini humo.

Bunge la Lebanon liliidhinisha mnamo mwezi Machi mkopo wa dola za Kimarekani milioni 246 kutoka Benki ya Dunia ambayo itatoa msaada wa pesa taslimu kwa zaidi ya familia 160,000.

Hata hivyo uamuzi huo ulicheleweshwa kutokana na hatua ya serikali kutaka kulipa familia maskini kwa pauni za Lebanon badala ya dola za Kimarekani.Zaidi ya nusu ya idadi jumla ya watu nchini Lebanon wanaishi katika umaskini mkubwa.