NA VICTORIA GODFREY, DAR ES SALAM

LIGI ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inatarajia kuendelea kuunguruma kwa michezo mitano kupigwa leo kwenye uwanja wa Habaours, Kurasini jijini hapa.

Michezo itakayochezwa ni ya wanaume JKT watavaana dhidi ya Outersiders itakayochezwa kwenye uwanja hui wakati JKT wakishuka dimba watakuwa na kumbukumbu ya kupigwa vikapu 85 – 76 na Ukonga Kings.

Hata hivyo Mgulani JKT watamenyana dhidi ya Ukonga warriors,huku Mchenga watashukz dimbani dhidi ya Jogoo, wakati DTB watatupa karata yao dhidi ya Savio,huku upande wa mtanange wa wanawake JKT Stars watapambana dhidi ya VBQ.

Michezo ya kesho kwa wanawake JKT Stars watafungua dimba dhidi ya Kurasini Divas,huku Ukonga Queens watavaana dhidi ya Mgulani Stars itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa DonBosco Upanga,Dar Es Salaam.

Kwa wanaume Kurasini Heat watashuka dimbani dhidi ya DTB,huku Chui watavaana dhidi ya Oilers na kumalizika mtanange wa Pazi watamenyana dhidi ya Maafande wa ABC kwenye dimba hilo.