TURIN, Italia
KOCHA Mkuu wa Juventus, Massimiliano Allegri, amesema, nyota wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo hataondoka msimu huu baada ya mazungumzo baina ya pande mbili.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 36, aliandika kwenye ukurasa wake kuwa kuhusishwa kung’oka Juve ni sawa na kumkosea heshima kama mwanadamu na mchezaji.
Akizungumzia kuelekea mechi za ligi, kocha Allegri, alisema, nahodha huyo wa Ureno atabakia.

“[Ronaldo] hajawahi kuonyesha nia ya kuondoka klabuni hapa, ameniambia anataka kubakia”, alisema, kocha huyo.
Juventus ilitarajiwa kufungua pazia la Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’ dhidi ya Udinese jana.

Katika siku za karibuni, Ronaldo amekuwa akihusishwa kujiunga na miamba ya soka ya Ufaransa, Paris St-Germain, Manchester City na kurejea Real Madrid ingawa yeye mwenyewe alikanusha hali kadhalika kwa kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti. (AFP).