NA MWANAJUMA MMANGA

TAASISI husika zimeombwa kuendelea kutoa elimu kwa madereva juu ya matumizi sahihu ya alama za barabarani, ili  zitumike Kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Wakizungumza na mwandishi wa gazedi hili watumiaji wa barabara kwa miguu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wamelalamikia baadhi ya madereva kutothamini alama za barabarani Jambo linalowapelekea kusababisha ajali kwa wapita njia.

Walisema wamekuwa wakiogopa hata kukata njia katika maeneo yenye alama za ZEBRA ambazo zimewekwa maalum kwa wanaoenda kwa miguu kutokana na madereva kutoziheshimu kabisa alama hizo na kusababisha ajali.

Aidha alifahamisha kuwa kuna baadhi ya madereva hasa waendesh boda boda kutosimama katika ZEBRA jambo ambalo limekuwa linaogopesha kwa wazee, walemavu na hata watu watoto ambao washapata elimu ya barabarani walizokuwa wakitoa (trafiki maskulini).

”Mdereva wengi siku hizi wamekuwa hawafuati alama ambazo zinaonyesha kila moja na matumizi yake huwa madereva wanazipuuza kwa kisingizio wanawahi kupita kukimbilia safari zake lakini cha kushangaza kusababisha ajali kwa uzembe” alisema kwa masikitiko.

Hivyo aliwasihi madereva kuwa waangalifu wakati wanapopita katika taa za barabarani na ZEBRA ili kuepusha ajali zisizokuwa za ulazima.

Kwa upande wao madereva wamesema baadhi ya alama hizo zimefutika kabisa hivyo ni vyema kwa taasisi husika ikaweka utaratibu wa kuzitia rangi kila baada muda, ili kuepusha lawama na kutokea kwa ajali zisizokuwa za lazima.

Akizungumzia kuhusu suala hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib Kamishna Msaidizi wa polisi, Awadhi Juma Haji, aliwataka madereva kufuata Sheria za alama za barabarani kwani Sheria zinamlazimu Dereva kuzifuata ambazo zimewekwa kutokana na umuhimu wake.