NA MWAJUMA JUMA

MAFUNZO ya awamu ya tatu ya makocha wa makipa  inatarajiwa kuanza kufanyika Agosti 15 mwaka huu.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) yatakuwa ya wiki moja, yataendeshwa na mkufunzi Saleh  Machupa anaetambulika na Shirikisho la Soka Africa (CAF).

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkufunzi huyo alisema jumla ya makocha 30 wanatarajiwa kushiriki mafunzo hayo ambayo yatafanyika katika uwanja wa Amaan.

Alisema makocha ambao watashiriki kozi hiyo ni wale walisoma mafunzo ya awali ya kwanza na pili kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Alifahamisha kwamba mafunzo hayo yatakuwa na kiingilio cha shilingi 230,000 atakayefaulu atapata cheti ambacho kitatambuliwa Tanzania nzima.