NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI Heritier Makambo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.Makambo aliwahi kuitumikia timu hiyo msimu wa 2018/19.Kwenye ukurasa wa kijamii wa klabu ya Yanga wa ‘Instagram’ waliandika kuwa mchezaji huyo Mkongo tayari amesaini akitokea kwenye kikosi cha Horoya FC ya nchini Guinea.

Mchezaji huyo inadaiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wanajangwani hao .Makambo yupo chini ya aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera ambaye pia ni raia wa Congo.

Makambo alitua Bongo juzi kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Yanga na baada ya kukamilisha utaratibu wa mwisho amesaini ndani ya timu hiyo ambayo inajiimarisha kwa ajili ya msimu ujao na itashiriki ligi ya mabingwa Afrika.