ANKARA, UTURUKI

WAOKOAJI wa Kituruki wameanza kuwahamisha mamia ya wakaazi wa vijiji kupitia baharini baada ya mto mbaya na hatari wa msituni kuyagubika maeneo yanayokizunguka kiwanda na kufua umeme kinachohifadhi maelfu ya tani za makaa ya mawe.

Maofisa wa zima moto na polisi wameonekana wakikimbia kutoka kiwanda cha Kemerkoy katika mkoa wa Mugla eneo la Aegean wakati moto mkubwa ulipokuwa ukiendelea kuwaka katika vilima vinavyolizunguka eneo hilo.

Mamia ya wanakijiji, wengi wao wakiwa wamebeba mikoba midogo yenye vitu vyao walivyovichukua kutoka makaazi yao, walianza kupanda kwenye boti za mwendo kasi karibu na bandari ya Oren.

Maofisa wa eneo hilo walisema kemikali zote zinazoweza kuripuka na nyenzo nyengine hatari zishaondolewa kutoka kwenye kiwanda hicho cha kimkakati.