LONDON, England

MANCHESTER UNITED iko tayari kumuuza Anthony Martial kwa Inter badala ya mkopo kwa mujibu wa taarifa.

Mabingwa wa Serie A wako kwenye mpango wa kumuuza Romelu Lukaku kwenda Chelsea kwa dau la pauni milioni 97.5, wakati Lautaro Martinez pia amehusishwa na kuondoka.

Inter bado inataka kuendelea kuwa na mkongwe wa Roma Edin Dzeko na Joaquin Correa wa Lazio, huku  Martial akiwindwa na klabu hiyo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa The Sun, Inter wanatarajia kumleta Mfaransa huyo kwa mkataba wa mkopo wa msimu wa kwanza, ingawa United inataka kwa  mkataba wa kudumu, kwani wanatafuta  fedha za kuimarisha timu yao.

Mashetani Wekundu tayari wametumia pesa nyingi msimu huu wa joto  kuwasajili Jadon Sancho na Raphael Varane, lakini bado wanataka kuleta beki wa kulia na kiungo mkabajia.

Inter na United wana uhusiano mzuri  na Lukaku, Ashley Young na Alexis Sanchez wote wamehama kutoka Manchester kwenda Milan na mazungumzo yanatarajiwa kwenda sawa.

Martial  hivi sasa anapata karibu pauni 200,000 kwa wiki na United ingekuwa na hamu ya kupata fedha nyingi kutoka kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25.