NA VICTORIA GODFREY

CHAMA cha Taekwondo mkoa wa Dar es Salaam (DTA) kinatarajia kuandaa mashindano ya wazi ya  watoto chini ya miaka 18 ambayo yamepangwa kufanyika Oktoba 16, mwaka huu jijini hapa.

Akizungumza na Zanzibar leo, Katibu Mkuu wa DTA Erasto Golyama,alisema walengwa katika mashindano hayo ni watoto wa skuli  za msingi na sekondari na kwamba wamelenga kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto ambavyo vitaandaliwa kwa hazina ya baadaye.

“Haya mashindano huwa tunaanza kila mwaka  tunashirikosha rika zote ,lakini mwaka huu tutakuwa tofauti tutashirikisha watoto tu ,tukiwa na lengo la kuutangaza mchezo na kukuza vipaji kuanzia ngazi ya chini,” alisema Golyama.

Katibu huyo alisema kuwa wanatarajia kutoa mialiko kwa skuli za mikoa ya Arusha,wilaya ya Moshi, Mombasa nchini Kenya na mingine  ili watoto waje kuungana kushiriki katika kusaidia kuinua na kuutangaza mchezo huo pamoja na kujifunza changamoto kutoka kwa wengine.

Aliongeza kuwa maandalizi yanaendelea kufanyika ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa weledi na kuleta mafanikio yaliyokusudiwa