YAOUNDE, Cameroun
JOEL Matip, amekataa wito mwengine wa timu ya taifa ya Cameroun, baada ya kustaafu mnamo 2016, huku akizingatia tu mambo ya klabu na Liverpool.

Matip aliamua kustaafu kuichezea Cameroun kabla ya kuondoka Schalke kwenda Liverpool, lakini, alionekana kwenye kikosi cha Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
Beki huyo wa kati, mzaliwa wa Ujerumani, alikuwa hajalijuulisha rasmi Shirikisho la Soka la Camerouni juu ya kustaafu kwake, ambapo ilimfanya akose michezo miwili ya Liverpool katikati ya msimu wake wa kwanza.

Hapo mwanzo, Matip alielezea kwamba alitaka ‘kuizingatia Liverpool’, ingawa inasemekana mara kwa mara kwamba uzoefu wake mbaya na timu ya taifa ulifikia uamuzi wake.
Ingawa majeraha yamekwamisha maendeleo yake huko Anfield, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ni mmoja wa mabeki bora wa kati kwenye Ligi Kuu ya England wakati akiwa fiti, na anaweza akawa mchezaji nyota kwa Cameroun.

Kwa hivyo haishangazi kwamba meneja, Toni Conceicao ambaye amekuwa akiisimamia tangu 2019, alitaka kumkumbuka Matip wakati wa uteuzi wake, bila ya kufaulu.
“Hali ya Matip sio mpya,” alielezea kabla ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia la Cameroun dhidi ya Malawi na Ivory Coast.

“Kuna wachezaji ambao walitaka kurudi kwenye timu ya taifa. Kwangu hakuna haja ya kumjumuisha mchezaji ambaye hayuko tayari kurudi.
“Matip hataki kurudi katika timu ya taifa, hilo ndilo suala”.(Goal).