PARIS, Ufaransa
BOSI wa Paris Saint-Germain, Mauricio Pochettino, amesema, Lionel Messi atakuwa sehemu ya kikosi kwenye mchezo wa wiki inayokuja dhidi ya Reims kwa mechi ya ‘Ligue 1’.
Baada ya kupata ushindi kwenye mechi tatu mfululizo za ufunguzi, PSG sasa ipo juu ya msimamo na inazidi kuimarika licha ya kukosekana kwa wachezaji nyota kama Messi na Neymar.

Hali hiyo haijaleta upungufu wowote zaidi ni kwamba tajiri amekwenda kuwa tajiri zaidi pale wachezaji hao wawili watakapoungana huku timu pia ikisajili kipa mpya, Gianluigi Donnarumma ambaye naye alikaa benchi kwenye mchezo waliyoshinda 4-2 dhidi ya Brest.

“Wiki imekuwa nzuri kwa Messi, kwa hiyo tunatumai wiki ijayo anaweza kuisadia timu na atajumuishwa kwenye kundi kwa ajili ya ushindani”, Pochettino aliiambia ESPN.
Beki Achraf Hakimi na Georginio Wijnaldum wamecheza michezo yote mitatu baada ya kujiunga na miamba hiyo ya Ufaransa.Lakini, Messi, Donnarumma na Ramos bado hawajacheza mchezo wowote na Ramos hatocheza mpaka baada ya mapumziko ya kimataifa.(Goal).