KAMPALA, UGANDA

MAWAKILI  nchini Uganda wamepinga maagizo ya Rais Museveni kwamba taasisi zinapaswa kuacha kuwakatisha tamaa wanasayansi ambao wanafanya juhudi kuja na uvumbuzi wa mafanikio ya mapambano ya janga la Covid-19.

Museveni, katika hotuba yake kwa njia ya televisheni kwa taifa wakati akizungumza juu ya juhudi kubwa zinazofanywa na wanasayansi kukuza matibabu ya Covid-19 alisema, muhimu kulinda haki miliki za wanasayansi waliohusika.

“Hawa ni wanasayansi waliowagundua ikiwa taasisi zinazoajiri wanasayansi hawa wanataka kufaidika na ubunifu wao, wanapaswa kulipia ushuru wa aina fulani, ambayo wataalamu wa uhamishaji wa teknolojia wanataja kama kugawana mirabaha.Hata hivyo, mapato mengi yanapaswa kwenda kwa mvumbuzi, ili tuwahimize wanasayansi wetu kugundua zaidi, ”akaongeza.

Kando na Prof Patrick Engeu Ogwang, mwanzilishi wa dawa ya matibabu ya Covid-19 Covidex, dawa nyengine ya mitishamba kusaidia matibabu ya Covid-19, Covilyce-1 imetengenezwa na Dk Alice Lamwaka kutoka Chuo Kikuu cha Gulu, na wote wana athari ya moja kwa moja kwa virusi.

Amri kutoka kwa Rais juu ya kulinda wanasayansi ilitolewa wiki chache baada ya mashitaka mawili ya sheria kuwasilishwa dhidi ya Prof Ogwang juu ya umiliki wa Covidex.

Prof Ogwang hakubaliani na mamlaka ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Mbarara juu ya umiliki wa dawa za mitishamba.

Mapema mwezi huu, wakili anayehusika George William Alenyo, na Chama cha Wafanyabiashara, Kilimo, Viwanda, Biashara na Utalii, walimshtaki Prof Ogwang akitaka matamko ya Mahakama kwamba dawa ya Covidex ni hati miliki ya serikali kwa kuwa ilitengenezwa kwa pesa za serikali , majengo na maabara.

AFP inabainisha kuwa Rais mwenyewe alisaini Sheria ya Mali ya Viwanda kuwa sheria ambayo sasa ni sheria inayosimamia suala lililopo.