NA HAFSA GOLO

MWAKILISHI wa Jimbo la Paje, Dk. Doud Nahoda Hassan, amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) na viongozi kuendelea kuhamasisha uimarishaji wa chama sambamba na ulipaji wa ada.

Alieleza hayo huko Bwejuu wakati alipokua akizungumza na wanaCCM wa jimbo hilo katika kikao cha kutathmini utekelezaji wa ilani.

Alisema ni vyema viongozi waongeza kasi ya kufanya kazi ya chama pamoja na mikutano kwa mujibu wa katiba na kanuni zinazowaongoza chama na jumuia kutika utekelezaji wa jambo hilo.

Aidha, alisema mikutano itasaidia kuibua hoja na mbinu mbadala ambazo zitazojenga utendani ndani ya chama na jumuiya zake.

“Tutapokuwa na michango mbali mbali katika ngazi tofauti italeta ufanisi juu ya uwajibikaji sambamba na uimarishaji wa chama chetu”,alisema

Alifahamisha kwamba utaratibu huo uendane na mikakati ya kusaidiana katika matokeo mbali mbali ya kijamii ikiwemo masuala ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.

“Tutaposhirikiana katika matokeo ya majanga na ujenzi wa miradi ya maendeleo katika shehia zetu upo uwezekano kwa kutimiza malengo tuliojiwekea”,alisema.

Nae Katibu Khamis Faki alisema kwamba suala la ulipaji wa ada ni jambo muhimu kwani humfanya mwanachama kuwa hai.

Hata hivyo, alisema ni vyema kwa viongozi wa jimbo kuandaa mafunzo maalumu kwa vijana yanayohusiana na historian a uzalendo  kila baada ya miezi sita.

Alifahamisha hatua hiyo italeta hamasa na mwamko kwa vijana hao katika kujitolea kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.