ZASPOTI
RAIA wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania, Malaika Mihambo, amelishindia taifa lake medali ya dhahabu katika mashindano ya michezo ya Olimpiki ya kuruka juu.

Mwanaridha huyo aliruka urefu wa mita saba na kuchukua ushindi.
Awali Mihambo alikabiliwa na changamoto kadhaa kabla ya mashindano hayo, lakini, hatimaye alifanikiwa kuonesha umahiri wake.
Katika fainali ya mchezo huo, Malaika hakuonesha ishara zozote za kuibuka mshindi.

Urefu wa mita saba alioruka katika jaribio la sita ulimwezesha kuipatia Ujerumani nishani yake ya kwanza ya dhahabu katika mchezo huo tangu Heike Drechsler aliposhinda mwaka 2000.

Nishani ya fedha ilimwendea mshindi mara nne wa mashindano ya dunia na Olimpiki yaliofanyika mjini London, Brittney Reese wa Marekani baada ya kuruka mita 6.97 huku Ese Brume wa Nigeria akijinyakulia medali ya shaba na kuiongezea Afrika idadi ya medali katika michezo hiyo.(Goal).