ZASPOTI
MWANARIADHA wa Kenya, Mark Otieno Odhiambo ameondoshwa nje ya mashindano ya Olimpiki ya Tokyo baada ya vipimo kuonesha ametumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa ametakiwa kushindana katika mbio za mita 100 za wanaume, lakini, alishindwa katika hatua ya vipimo na kubainika alitumia dawa za kusisimua misuli.

Kwa mujibu wa mkuu wa msafara huko Tokyo Waithaka Kioni: “Hata hivyo amekataa kutambua madai ya ukiukaji huo na kuomba uchambuzi wa sampuli yake ya mkojo .”
Kipimo kilifanyika Juni 28 wakati mwanariadha huyo alipokuwa Tokyo, kabla ya hapo alikuwa kwenye kambi ya mazoezi nchini Japan kati ya tarehe 15 na 24 mwezi Julai.
Otieno Odhiambo alishiriki kwenye Mashindano ya Dunia ya 2017 na Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2018.

Ni mwanariadha wa pili wa Kiafrika kuondolewa kwenye michuano hiyo baada ya nigeria, Blessing Okagbare.
“Haya ni mambo ambayo labda yanaweza kuepukika hii ndio sababu inaendelea kuwasiliana na mashirikisho ya michezo na ADAK kwa hivyo tunaendelea kutoa elimu juu ya kupambana na dawa zilizopigwa marufuku kwa wanariadha wetu, “aliiambia, BBC Sport Africa.

“Lakini sio kwamba wanariadha hawajui na ndio sababu tunachukulia kuwa hana hatia hadi tutakapochunguza tena sampuli ‘B’ ya mkojo.
“Nilizungumza naye mchana huu na ananiambia hawezi kukumbuka kama alitumia kitu chochote ambacho kitatoa matokeo ya aina hiyo.
“Kinachonisumbua ni kwamba Kenya tayari imekuwa kwenye orodha ya waliowekewa alama nyekundu na tulitarajia tutatoka katika orodha hiyo, lakini, tukio kama hili linaweza kuvuruga mpango wa kujinasua”.(BBC Sports).