VIENNA, AUSTRIA
SUALA la wakimbizi kutoka Afghanistan limesababisha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa nchi za Ulaya, ambao umedhihirika katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi wanachama wa umoja huo.
Waziri wa mambo ya ndani wa Austria Karl Nehammer amepinga vikali wazo la kuwakaribisha wakimbizi hao barani Ulaya, akisisitiza badala yake kuundwa kwa vituo vya wakimbizi wa Afghanistan katika ukanda wa Asia ya kati.
Waziri huyo pia ameshikilia msimamo wa nchi yake wa kuendelea kuwafukuza wahamiaji raia wa Afghanistan ambao maombi yao yalikataliwa.
Ugiriki iliunga mkono msimamo huo wa Austria.
Kwa upande mwengine, waziri wa Luxembourg Jean Asselborn alipendekeza nchi za Ulaya zikubaliane idadi ya wakimbizi Waafghanistan watakaokubaliwa Ulaya.
Kamishna wa masuala ya ndani ya Umoja wa Ulaya Ylva Johansson ametaka ibuniwe njia ya kuwawezesha wakimbizi kutoka Afghanistan kufika barani Ulaya.