PARIS, Ufaransa

MECHI ya ligi ya Ufaransa kati ya wapinzani Nice na Marseille haikumalizika juzi Jumapili usiku baada ya wafuasi wa Nice  kurusha makombora kwa wachezaji uwanjani, na kuzua tafrani kali kati ya wachezaji, mashabiki na wafanyikazi.

Kiungo wa kati wa Marseille, Dimitri Payet alipigwa mgongoni na chupa iliyotupwa kutoka eneo lenye mashabiki wa Nice kuelekea mwisho wa mchezo na nyota huyo wa zamani wa West Ham alianguka kabla ya kunyanyuka kwa hasira kuirejesha chupa hiyo kwa mashabiki.

Tukio hilo lilishuhudia mashabiki kadhaa wa Nice, ambao hapo awali walikuwa wameonywa dhidi ya kutupa vitu na mtangazaji wa uwanja, wakikimbilia uwanjani kumpiga Payet, na picha zilionekana kuonyesha mfanyakazi mmoja wa Marseille alipigwa na kuvamiwa hafla.

Pamoja na idadi kubwa ya mashabiki kumwagika uwanjani, mwamuzi alisimamisha mechi wakati wachezaji wa Marseille waliingia kuingilia kati, wakikabiliana na wafuasi wa Nice wenye hasira.

Timu zote mbili zilirudi kwenye vyumba vya wachezaji kabla ya mwamuzi Benoit Bastien kutangaza kuvunja mchezo, wachezaji wa Nice walikuwa wamerudi uwanjani dakika kadhaa mapema wakati wachezaji wa Marseille walikataa kurudi