LAGOS, NIGERIA

RAIS wa zamani wa Nigeria ameteuliwa kuwa mjumbe wa Umoja wa Afrika katika eneo la Pembe ya Afrika.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat, alitangaza hapo juzi kwamba Rais wa zamani wa Nigeria. Olusegun Obasanjo, atazidisha mazungumzo na wahusika wote wa kisiasa na wadau katika eneo hilo ili kuimarisha amani na utulivu ndani ya Pembe ya Afrika.”

Aliongeza kuwa, Obasanjo atawasili katika eneo hilo katika wiki zijazo na Umoja wa Afrika umeziomba pande zote kumuunga mkono.

Uteuzi wake umekuja wakati wa ghasia za kisiasa na usalama katika eneo hilo, hasa nchini Ethiopia, ambako makao makuu ya Umoja wa Afrika yanapatikana.

Haya yanajiri baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano na vitendo vya uhasama nchini Ethiopia.