WARSHAWA, POLAND

POLAND ina mpango wa kujenga uzio katika mpaka wake na Belarus na kupeleka wanajeshi zaidi ili kuzuia wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya.

Serikali ya Poland ilisema imejitolea kutuma misaada ya kibinadamu kwa wahamiaji waliokwama kwenye mpaka wa nchi hiyo kwa zaidi ya wiki mbili.

Poland na mataifa ya Baltic yakiwemo Latvia, Lithuania na Estonia, yamemshutumu rais wa Belarus Alexander Lukashenko kwa kutuma kwa makusudi wahamiaji katika mipaka ya nchi hiyo ambayo ni sehemu ya mpaka wa mashariki wa Umoja wa Ulaya.

Wahamiaji wengi wanatokea Afghanistan na Iraq.Mataifa hayo yanaamini kuwa ongezeko la wahamiaji katika mipaka yake ni mojawapo ya njia za kulipiza kisasi kwa Belarus kwa kuwekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya.