NA TATU MAKAME

TATIZO la maji safi na salama katika kisiwa cha Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja, bado  ni kero inayowakabili wananchi wa kisiwa hicho kwa muda mrefu hivi sasa.

Wananchi wa kijiji hicho walisema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Ayuob Mohamed Mahmoud, katika kikao kilichowashirikisha wazee wa kijiji hicho na watendaji wa Ofisi ya Mkoa ikiwa ni muendelezo wa ziara za Mkuu huyo kusikiliza kero za wananchi.

Walisema kero hiyo ni ya muda mrefu, ambayo inahitaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka, ili kondosha matatizo hayo kijijii hapo, kwani walisharipoti kwa wakuu wa mamlaka zinazohusika, lakini bado changamoto hizo hazijapatiwa ufumbuzi.

Hassani Mwadini Haji na Hamadi Haji Nyange, walisema katika kisiwa cha Tumbatu wanakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama pamoja na uvuvi haramu kwa kipindi kirefu, hali inayosababisha kero kwa wakaazi wa kijiji hicho.

“Matatizo hayo yasiposhuhulikiwa ipasavyo yataondosha uimarikaji wa ustawi wa jamii zetu sisi wananchi wa kisiwa cha Tumbatu”, alisema.